KISWAHILI SANIFU
Bwana Maina Muhindi
|
|
|
|
|
Baada ya siku nyingi huko
Afrika Kusini., ameingia London
CLICK HERE FOR - Methali za kiswahili ---- Swahili proverbs
KISWAHILI SANIFU
METHALI ZA KISWAHILI
1. Ada ya mja, hunena: muungwana ni kitendo
2. Adui mpende.
3. Afua ni mbili, kufa na kupona.
4. Akomelepo mwenyenji na mgeni koma papo.
5. Ajali haina kinga.
6. Aliye juu yu juu.
7. Aliye kando haangukiwi na mti.
8. Aliyepeleka mkono kutamalaki si kazi.
9. Anipendaye nami nampenda, anikataye, napunguwa simanzi.
10. Anipendaye nami nampenda, anitakaye, napunguwa simanzi.
TANAKALI ZA SAUTI
1. Giza totoro.
2. Kweupe pepepe.
3. Kufa fofofo.
4. Mweusi tititi.
5. Nyeupe pepepe.
6. Kunyamaza jii.
7. Kujaa pomoni.
8. Kukataa kata kata.
9. Kutulia tulii.
10. Kunyooka twa.
TAKRIRI
1. buheri wa afya
2. balaa na beluwa
3. dhahiri shahiri
5. bure bilashi
6. daima dawamu
7. miaka na dahari
8. harusi wala matanga
9. togo wala jando
10. uso kwa macho
MISEMO
kupiga
kupiga pasi
kupiga domo
kupiga mbizi
kupiga picha
kupiga ngoma
kupiga kelele
kupiga kofi
kupiga simu
kupiga ramli
kupiga kilemba
kupiga kafi
kupiga chafya
kupiga zumari
kupiga miyao
TASHBIHI
1. Kuadimika kama wali wa daku.
2. Kubahatika kama mwana aliyezaliwa Ijumaa.
3. Kubaidika kama ardhi na mbingu.
4. Kudahadari kama mtu anayetoka roho.
5. Kuganda kama kigaga.
6. Kujitia katikati kama mchuzi wa ugali.
7. Kukonda kama ng'onda.
8. Kuwa na miguu mirefu kama korongo.
9. Kuwa na shingo nene kama mbuyu.
10. Kuwa na maneno mengi kama chiriku.
SEMI ZA KISWAHILI
( coming soon)
JAMAA
ami - kaka yake baba yangu
baba - mzazi wangu wa kiume
baba mkwe - baba yake mke wangu
baba wa kambo - mume wa mama yangu lakini si baba mzazi
babu - baba yake mama
bibi - mama yake mama
binti - mtoto wa kike
dada - mtoto mwanamke wa mama
kaka - mtoto mwanamume wa mama
RANGI
mifano
chanikiwiti rangi ya samli
kijani rangi ya sneri
kijani kibichi rangi ya udongo
waridi rangi ya fedha
majano rangi ya dhahabu
manjano mabichi hudhurungi
majano mwangaza samawati
MAJINA YA MAKUNDI
1. Umati wa watu
2. Furushi la nguo.
3. Tita la kuni.
4. Darasa la wanafunzi.
5. Koja la maua.
6. Jozi ya karata.
7. Kundi la ng'ombe.
8. Kifungu cha mchanga.
9. kichaka cha miti.
10. Mkururo wa watoto.
WATU MBALI MBALI
1. kibogoyo - mtu asiyekuwa na meno
2. bubu - mtu asiyeweza kusema.
3. kibyongo - mtu mwenye nundu mgongoni.
4. kiwete - mtu aliyelemaa miguu.
5. mja - mzito - mwanamke mwenye mimba.
6. kiguru - mtu mwenye mguu mbovu na anakwenda kwa kuchechemea.
7. kiziwi - mtu mwenye masikio mabovu asiyeona.
8. kipofu - mwenye macho mabovu asiyeona.
9. chongo - mtu ambaye jicho lake moja tu ndilo linaloona.
10. mwenda - wazimu - mtu asiye na akili timamu.
WAFANYIKAZI
Mfanyakazi Kazi
Mchuuzi Mtu anayeuza vitu rejareja.
Mfinyanzi Mtu anayefanza vyungu na vyombo vingine kwa udongo.
Mganga Mtu ajuaye habari za madawa na kuzitumia kuponyesha watu.
Mgema Mtu apandaye mnazi kukata karara lake ili kutoa maji yake, yaani tembo.
Mhunzi Mfua chuma.
Mjumbe Mtu aliyetumwa.
Mkalimani Mtu aelezaye maneno ya lugha moja kwa lugha nyingine kwa kusema, si
kwa kuandika.
Mwezekaji Fundi wa kuezeka nyumba.
Mwizi Mtu aibaye, achukuaye vitu vya watu bila ya ruhusa.
Muuguzi Mtunzaji wagonjwa.
VYOMBO
kasiki mtungi
gudulia sufuria
chungu karai
legeni sinia
sahani bakuli
bilauri buli
birika debe
chano ungo
kikango kandili
kibatari chupa
susu pakacha
kikapu gunia
kasha sanduku
tasa mkoba
mfuko ala
kata pipa
kikombe seredani
tanuri kisima
kidawa kibeti kabati
MASHAIRI
1. FITINA
Mara nyingi, sisi binadamu twatumbukia kwenye mtumbwi wa mfinyanzi na kubanwa na
biwi la simanzi kwa msiba wa kujitakia wenyewe. Ni dhahiri shahiri ya kwamba
baadhi yetu ni vibilifitina na kina pangu pakavu tia mchuzi. Mara kwa mara,
twahatarisha maisha ya ndugu zetu kwa kuwaonea wivu na kuwafitini bure.
Ndiposa leo hii najibwaga katika ukumbi huu wa sanaa kwa
kurejelea shairi murua la msanii
Rwechungura. Tafadhali jumuika nami na ulisome kwa fahamu na sina shaka utafaidi.
Bwana Muhindi.
FITINA
Fitina mtu khatari, siwezi kukhadithia,
Mzushi hana nadhari, mjasusi wa kuzua,
Anuka kama jodari, papa bovu la India,
Fitina mvunja mji, umwonapo tahadhari.
Fitina hana jeuri, usoni huchekelea,
Hudai hana kiburi, laghai kunyenyekea,
Hujifanya yu tayari, kitini kukwinukia,
Fitina mvunja mji, umwonapo tahadhari.
Fitina mtu ayari, heshi kukutembelea,
Si mwema na si mzuri, hakai akatulia,
Upole akuvinjari, apate kukuzulia,
Fitina mvunja mji, umwonapo tahadhari.
Fitina mfano ngiri, heshima hajatambua,
Domo halitaghairi, kutoa yasio njia,
Hata awe mshairi, fitina wote sawia,
Fitina mvunja mji, umwonapo tahadhari.
Fitina hana bahiri, maneno kupangilia,
Fitina hana dosari, zaidi ya laki mia,
Fitina katika pori, hukaa akangojea,
Fitina mvunja mji, umwonapo tahadhari.
Fitina si urafiki, ni utovu wa tabia,
Halimukhusu fikiri, kwa nini kushikilia,
Na kufanya dhamiri, kukaa kusimulia,
Fitina mvunja mji, umwonapo tahadhari.
Fitina khasa kafiri, karibu mwenye kuua,
Huzikusanya khabari, kila pembe ya dunia,
Uulizapo hakiri, adui wa watu pia,
Fitina mvunja mji, umwonapo tahadhari.
Fitina leo kariri, usome ukirudia,
Ndoa ikisha shamiri, huwezi kuitangua,
Ila atake Kahari, wakati ukiwadia,
Fitina mvunja mji, umwonapo tahadhari.
Fitina hii nadhiri, siku moja tatimia,
kugundua ikijiri, kifungo nitachukua,
Fitina hata tajiri, ras yake taitoa,
Fitina mvunja mji, umwonapo tahadhari.
INSHA / HADITHI ZA KUBUNI
(soon)
VITENDAWILI
( soon)
MASWALI NA MAJIBU
(soon)